JOHANNESBURG: Wasichana 7 wamezama pwani
22 Mei 2005Matangazo
Wasichana 7 wamezama nchini Afrika ya Kusini na 1 bado anakosekana,baada ya kikundi cha wanafunzi kwenda kuogelea baharini.Ajali hiyo ilitokea mapema asubuhi,baadhi ya wanafunzi walipoamua kwenda kuogelea,hata kabla ya walinzi wa pwani kufika kazini.Kiasi ya wanafunzi 300 wakifuatana na walimu,walikwenda pwani baada ya kuhudhuria michezo ya spoti huko Richard´s Bay mashariki mwa nchi.Helikopta na boti za uokozi zinamsaka msichana wa nane ambae bado hajaonekana.