JOHANNESBURG:Mjane wa kiongozi wa ANC wa zamani afariki
1 Februari 2007Mjane wa kiongozi wa zamani wa chama cha African National Congress ANC Oliver Tambo amefariki.Bi Adelaide Tambo aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 77 akiwa nyumbani mwake mjini Johannesburg wakati wa jioni.
Bi Tambo aidha alikuwa mwanaharakati wa kisiasa na kutazamwa kama mama kwa wanasiasa waliokuwa uhamishoni wakati wa kipindi cha uongozi wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
Bwana na Bi Tambo walifunga ndoa mwaka ’56 na kuishi uhamishoni kuanzia mwaka ’60.Oliver Tambo alikuwa kiongozi wa chama cha ANC akiwa uhamishoni wakati Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela alipokuwa kizuizuini.Bwana Tambo aliheshimika katika ngazi za kimataifa na kuungwa mkono ulimwenguni katika harakati za kuondoa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.Oliver Tambo alifariki mwaka 93 ,mwaka mmoja kabla nchi hiyo kufanya uchaguzi wake wa kwanza wa kidemokrasia pasipo ubaguzi wa rangi.Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini anatuma rambirambi zake kwa famila ya marehemu.