JOHANNESBURG:Naibu waziri wa afya kuilipa serikali
24 Agosti 2007Naibu waziri wa Afya wa zamani wa Afrika Kusini Nozizwe Madlala-Routledge ameamriwa kulipa gharama za safari aliyoifunga hadi Uhispania ili kuhudhuria mkutano wa Ukimwi.Bi Nozizwe Madlala –Routledge alifukuzwa kazini mwanzoni mwa mwezi huu kwasababu ya kufunga safari hiyo iliyogharimu dola alfu 42.
Hatua ya kuachishwa kazi kwake kumezua hisia tofauti miongoni mwa wanaharakati wa Ukimwi na vyama vya upinzani.Kulingana na wanaharakati hao Bi Nozizwe Madlala-Routledge alikuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya Ukimwi hususan sera za kupambana na ugonjwa huo zinazoegemea zaidi matumizi ya elimu ya sayansi.
Msimamo huo unatofautiana vikali na ule wa Waziri wa Afya Manto Tshabalala-Msimang anayeamini kuwa virusi vya HIV vinaweza kumalizwa na lishe bora pekee.Takriban raia milioni 5.5 wa Afrika Kusini wana virusi vya HIV