JOHANNESBURG:Rais Mkapa wa Tanzania ziarani Afrika Kusini
21 Septemba 2005Matangazo
Rais anayeondoka madarakani wa Tanzania Benjamin mkapa leo anaanza ziara yake ya siku tatu ya kiserikali nchini Afrika kusini kabla ya kung’atuka madarakani mwezi ujao.
Rais Mkapa atafanya mazungumzo na rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki juu ya masuala ya ushirikiano wa kisiasa na Uchumi kati ya nchi hizo pamoja na maendeleo katika eneo la Afrika ikiwa ni pamoja na hali mpya ya kisiasa nchini Burundi na Ivory Coast.
Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini nchi hizo mbili zinatarajiwa kutia saini makubaliano ya kuondosha vizingiti vya kibiashara.
Rais mkapa atatembelea Lesotho baada ya ziara yake nchini Afrika Kusini.