JOHANNESBURG.Serikali ya Afrika Kusini yaidhinisha ndoa kwa watu wa jinsia moja
15 Novemba 2006Matangazo
Afrika Kusini ni ya kwanza katika bara la Afrika kuidhinisha ndoa ya watu wa jinsia moja.
Wabunge 230 wametia saini mswaada wa kuidhinisha sheria hiyo huku wabunge 41 wakiupinga wakati ulipowasilishwa bungeni, wabunge watatu hawakushiriki.
Serikali ya Afrika Kusini ililazimika kubadili katiba ya nchi hiyo baada ya mahakama kuu ya nchi hiyo kutoa uamuzi kwamba watu wa jinsia moja na wanaotaka kuoana walinyimnwa haki katika katiba ya zamani.