John Heche ashtakiwa kwa ugaidi
5 Novemba 2025
Katika chapisho kwenye mtandao wa X, jana jioni, Chadema imesema kuwa Heche ambaye alikamatwa Oktoba 22, ameshtakiwa kwa "vitendo vya ugaidi".
Kinasema polisi ilimsafirisha Heche kutoka mji mkuu Dodoma hadi eneo la pwani la Kinodoni ambako alifunguliwa mashtaka hayo.
Taarifa hiyo pia imesema naibu mwenyekiti huyo alikataa kuandika taarifa lakini atafanya hivyo mara tu baada ya kufikishwa Mahakamani.
Haijabainishwa wazi ni lini atafikishwa mahakamani.
Mashirika ya haki yaelezea kukandamizwa kwa upinzani nchini Tanzania
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameelezea ukandamizaji wa kikatili dhidi ya upinzani kabla ya uchaguzi, huku viongozi wao wakifungwa jela au kuzuiwa kugombea.
Kiongozi wa chama hicho cha Chadema, Tundu Lissu, kwa sasa anakabiliwa na kesi ya uhaini ambayo inaweza kubeba hukumu ya kifo.