John Mahama ameapishwa kuiongoza Ghana
7 Januari 2025Matangazo
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni pamoja na rais Bola Tinubu wa Nigeria,Bassirou Diomaye Faye wa Senegal, Ibrahim Traore wa Burkinafaso, William Ruto wa Kenya na Felix Tschisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mahama alishinda kwa asilimia 56 ya kura katika uchaguzi wa rais uliofanyika Desemba 9 na kumshinda mgombea wa chama tawala na aliyekuwa makamu wa rais Mahamudu Bawumia aliyepata asilimia 41 ya kura.
Soma pia: Mahama arejea Ikulu ya Accra
John Mahama ameapishwa kumrithi rais anayeondoka Nana Akufo Addo ambaye ameiongoza Ghana kwa mihula miwili.
Jane Naana Opoku -Agyemang,nae ameapishwa kama makamu wa kwanza wa rais mwanamke nchini humo. Mahama amesema Ghana sasa imeanza kipindi cha fursa mpya za kujijijenga.