1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Johnson ashinda uchaguzi kukiongoza chama cha Conserative

23 Julai 2019

Boris Johnson anaelekea kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza baada ya kushinda kwa kishindo uchaguzi wa wanachama wa Conservative wa kumchagua kiongozi wao mpya.

Großbritannien London | Boris Johnson wird neuer Premierminister
Picha: Reuters/T. Melville

Waziri wa zamani wa mambo ya kigeni wa Uingereza Boris Johnson amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama tawala cha Conservatives nchini humo atakayechukua mara moja nafasi ya Bi Theresa May.

Hii inamaanisha Boris Johnson sasa atakuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza baada ya May kutangaza kujiuzulu mwezi uliyopita.

Boris aliye na miaka 55 alimshinda mpinzani wake Jeremy Hunt kwa wingi wa kura katika uchaguzi wa wanachama wa chama cha conservatives hii leo.

Waziri huyo wa masuala ya kigeni wa zamani wa Uingereza ananatarajiwa kuchukua rasmi nafasi hiyo ya uwaziri Mkuu hapo kesho Jumatano (24.07.2019).

Ingelikuwa mshituko mkubwa  iwapo uongozi huousingekwenda kwa Boris Johnson, meya  wa  zamani  wa  London ambaye  amewavutia  wanachama  wa  chama  cha  Conservative  kwa  kuahidi  kufanikisha  pale  ambapo  May  alishindwa  na  kuiongoza  Uingereza  kujitoa  kutoka  Umoja  wa  Ulaya katika  tarehe  iliyopangwa  Oktoba  31, kwa  kupata  makubaliano  ama  la.