1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jordan kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya mageuzi ya Syria

14 Desemba 2024

Jordan leo hii itakuwa mwenyeji wa Marekani, Umoja wa Ulaya na wanadiplomasia wa mataifa ya Kiarabu katika mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu Syria.

Syrien |  Damaskus Feierlichkeiten zum Sturz von al-Assad
Picha: SAMEER AL-DOUMY/AFP/Getty Images

Mkutano huo unafanyika siku moja tu, baada ya sherehe mjini Damascus na kote nchini Syria kufurahia kuangushwa kwa mtawala wa kiimla rais Bashar al-Assad. Kuanguka kwa Assad pia kumesababisha maendeleo ya haraka ya kidiplomasia, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa miongoni mwa wajumbe wanaotarajiwa kuijadili Syria leo hii katika mji wa Aqaba nchini Jordan. Mwanadiplomasia wa Qatar amesema wajumbe kutoka katika taifa la Ghuba watazuru Syriakesho Jumapili kukutana na maafisa wa serikali ya mpito na kujadili msaada na kufunguliwa tena kwa ubalozi wao. Na kadhalika Uturuki ikitangaza kuwa itaufungua tena ubalozi wake mjini Damascus, uliofungwa tangu mwaka 2012.Assad ameikimbia Syria, na kuhitimisha enzi ambayo watu wanaoshukiwa kuwa wapinzani walifungwa au kuuawa, na kumaliza karibu miaka 14 ya vita vilivyoua zaidi ya watu 500,000 na mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW