1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPanama

Jose Raul Mulino achaguliwa rais mpya nchini Panama

6 Mei 2024

Mwanasiasa Jose Raul Mulino amaechaguliwa usiku wa kuamkia leo kuwa rais mpya wa Panama.

Rais mteule wa Panama, Jose Raul Mulino
Rais mteule wa Panama, Jose Raul Mulino.Picha: Matias Delacroix/AP/picture alliance

Matokeo yametolewa saa chache baada ya kukamilika kwa uchaguzi uliogubikwa na kizaazaa kinachomkabili rais wa zamani wa taifa hilo ambaye alizuiwa kushiriki uchaguzi huo katikati mwa kipindi cha kampeni.

Mulino mwenye umri wa miaka 64 ameshinda kwa zaidi ya theluthi mbili ya kura zilizopigwa. Tangazo rasmi la ushindi huo limetolewa na tume ya uchaguzi ya taifa hilo la Amerika ya Kati.

Anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuondoa migawanyiko ndani ya jamii na kurejesha imani ya umma uliochoshwa na vitendo vya rushwa kwenye siasa za nchi hiyo.

Mulino, alichukua nafasi ya kuwa mgombea baada ya mshirika wake aliyewahi pia kuwa rais wa Panama, Ricardo Martinelli, kuzuiwa mnamo mwezi Machi kuwania uchaguzi huo baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la utakatishaji fedha.

Martinelli alikimbilia kwenye ubalozi wa Nicaragua nchini Panama na kupewa hifadhi lakini alibakia kuwa na ushawishi mkubwa kwenye kampeni za uchaguzi.