Joseph Kabila kuapishwa rais wa DRC kwa muhula mwingine
20 Desemba 2011Matangazo
Tshisekedi anashikilia hivyo, licha ya mahakama kuu nchini humo siku ya Ijumaa kuthibitisha kuwa rais wa sasa Joseph Kabila ameshinda kwa kupata asilimia 49 ya kura na Tshisekedi asilimia 32.
Umoja wa Afrika umeueleza uchaguzi huo kama ni mafanikio, lakini Umoja wa Ulaya, Kituo cha Carter chenye makao yake nchini Marekani na wasimamizi wengine wa uchaguzi wanasema, uchaguzi wa Novemba 28 ulikuwa na dosari.
Joseph Kabila anatazamiwa kuapishwa leo kwa awamu nyingine. Tshisekedi pia amejipangia sherehe ya kuapishwa siku ya Ijumaa.