Iran yatoa mapumziko ya siku mbili kutokana na joto kali
2 Agosti 2023Matangazo
Msemaji wa serikali Ali Bahadori Jarhomi amesema uamuzi wa kuzifunga ofisi za serikali, benki na shule leo na kesho Alhamisi umejiri baada ya wizara ya afya kuonya kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa visa vya uchovu kwa sababu ya joto kali. Katika siku za karibuni, miji nchini Iran imeshuhudia kiwango cha joto cha karibu nyuzijoto 40 za Celcius. Mji mkuu Tehran ulishuhudia nyuzijoto 38 za Celcius jana Jumanne. Idara ya Hali ya Hewa imetabiri kuwa Tehran itashuhudia kiwango cha nyuzijoto 38 za Celcius katika siku tatu zijazo. Mji wa Ahvaz, wa mkoa wa kusini magharibi mwa nchi hiyo wenye utajiri wa mafuta ulishuhudia nyuzijoto 50 za Celcius hapo jana.