1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juan Guaido apokelewa kwa shangwe aliporejea Caracas

Oumilkheir Hamidou
5 Machi 2019

Kiongozi wa upinzani wa Venezuela, Juan Guaido amepokelewa kwa shangwe aliporejea nyumbani licha ya hofu ya kukamatwa na kutoa wito wa kuitishwa maandamano makubwa jumamosi inayokuja kumshinikiza rais Nicolas Maduro.

Politische Krise in Venezuela Juan Guaido Kundgebung in Caracas
Picha: picture-alliance/dpa/F. Llano

"Jumamosi tutaendelea". Nchi nzima itateremka majiani. Hatutotulia si mpaka tunapata uhuru wetu" amesema Guaido mbele ya maelefu ya watu waliokusanyika katika uwanja mmoja mjini Caracas, muda mfupi baada ya kurejea.

Juan Guaido, aliyejitangaza rais wa mpito na kutambuliwa na nchi zisizopungua 50 aliondoka kwa siri Venezuela siku kama kumi zilizopita akielekea Colombia.

Alipowasili jana mchana mchana katika uwanja wa ndege wa Ccaracas, alipokelewa na wafuasi wake pamoja pia na ujumbe wa mabalozi wa nchi za magharibi na Latin Amerika waliokuja kudhamini usalama wake.

Juan Guaido akizungumza na waandishi habari baada ya kurejea CaracasPicha: Reuters/C. Jasso

Guaido anasema wamepania kuhakikisha mwisho wa enzi za Maduro

Wametutisha sote tuliofika hapa, watatufunga watatuuwa. Mmeona nyote. Mie nnawaambia kitu kimoja: "si adhabu na wala si vitisho vitakavyotuzuwia.Tumeshafika na tumeungana nguvu kuliko wakati wowote ule mwengine.Tuko na tuna nguvu kuliko wakati wowote mwengine."

Kabla ya ndege yake kutuwa mjini Caracas, makamo wa rais wa Marekani Mike Pence alimuonya rais Nicolas Maduro ahakikishe usalama wa Juan Guaido huku waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo akisifu baadae kurejea Guaido salama nyumbani."Jumuia ya kimataifa inabidi iungane ili kuhakikisha mwisho wa utawala wa kimabavu wa Maduro na kurejea amani na demokrasia nchini Venezuela amesema makamo nwa rais wa Marekani Mike Pence.

"Vitisho vya aina yoyote, matumizi ya nguvu au njama yoyote dhidi yake havitovumiliwa na vitajibiwa vikali" amesema Mike Pence kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: picture-alliance/KEYSTONE/S. Di Nolfi

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres ahimiza majadiliano

Hatari ya kukamatwa bado ingalipo" anaonya senetor wa Marekani Marco Rubio na kuongeza huenda Guaido akakamtwa atakapokuwa peke yake bila ya kuzungukwa na wafuasi wake, waandishi habari na wanadiplomasia.

Rais wa Colombia Ivan Duque amesema kurejea nyumbani Guaido ni sehemu ya njia isiyobadilika kuelekea democrasia nchini Venezuela. Nae katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gueterres ametoa wito wa kuitishwa mazungumzo ya kisiasa ya pande zote ili kumaliza mvutano.

 

Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/AP/AFP

Mhariri: Mohammed Khelef

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW