JUBA: Majadiliano kati ya serikali ya Uganda na wajumbe wa LRA
16 Julai 2006Matangazo
Majadiliano ya amani,kati ya serikali ya Uganda na waasi wa Lord´s Resistance Army(LRA) yenye azma ya kumaliza uasi wa miaka 19 yameanza tena nchini Sudan.Mazungumzo hayo yalikwama siku ya Jumamosi baada ya tume ya serikali kutishia kuondoka mkutanoni kwa sababu ya hotuba ya msemaji wa LRA.Obonyo Olweny,alimtuhumu rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa mashtaka ya rushwa na akaonya kuwa kundi la LRA halijakubali kufanya majadiliano kwa sababu ya kuwa dhaifu kijeshi. Msemaji wa tume ya serikali ya Uganda,Paddy Ankunda ameeleza kuwa pande mbili zimekubaliana na sheria na utaratibu utakaoongoza majadiliano hayo.