JUBA:Viongozi wa waasi wa LRA wahofia kukamatwa !
9 Oktoba 2006Matangazo
Waasi wa Lord Resistance Army wa nchini Uganda wamesema kuwa hawatatia siani mapatano ya kuleta amani baina yao na serikali ya nchi hiyo ikiwa waranti juu ya kukamatwa viongozi wao hazitabatilishwa .
Wawakilishi wa waasi hao wanafanya mazungumzo na serikali ya Uganda kusini mwa Sudan juu ya kumaliza vita vilivyochukua muda wa miaka 20.
Mahakama ya kimataifa ya mjini the Hague imetoa waranti juu ya kukamatwa ,makamanda wanne wa kundi hilo la waasi ili kujibu tuhuma juu ya ukatili uliofanywa wakati wa vita hivyo.
Makamanda hao wanataka wapewe uhakikisho kuwa hawatakamatwa baada ya mapatano ya kuleta amani kutiwa saini.
Serikali ya Uganda haijasema chochote juu ya tashi la waasi hao .