1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za kutafuta upatanishi Mali zagongwa mwamba

24 Julai 2020

Juhudi za viongozi kadhaa wa Afrika Magharibi kuusuluhisha mzozo wa kisiasa nchini Mali zimegonga mwamba, baada ya pande zinazohasimiana nchini humo kukataa kujitokea kuleta maridhiano.

Frankreich Paris 2018 | Ibrahim Boubacar Keita, Präsident Mali
Picha: picture-alliance/dpa/Maxppp/Mousse

Rais wa Senegal Macky Sall, Alassane Ouattara wa Ivory Coast, Mahamadou Issoufou wa Ghana na Muhammadu Buhari wa Nigeria, waliongoza ujumbe wa upatanishi wakiwa pamoja na aliyekuwa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan katika mji mkuu wa Mali, Bamako.Kundi hilo kwanza lilikutana na rais wa Mali Ibrahim Boubakar Keita na kufuatia na mazungumzo na muungano wa makundi ya upinzani yanayomtaka Keita kujiuzulu. Lakini kufikia jana jioni, hakuna upande uliokuwa tayari kufanya makubaliano na kusababisha mkwamo katika juhudi hizo za upatanishi.

Baada ya mazungumzo hayo, muungano huo wa upinzani unaoongozwa na mhubiri maarufu Mahmoud Dicko, uliishtumu serikali ya Keita kwa uongozi mbaya huku msemaji wa upande wa Keita akisema kuwa wito wa kumtaka Keita kujiuzulu ni kinyume cha sheria.Raia wa Mali pia wameghadhabishwa na matokeo yanayotiliwa shaka ya uchaguzi wa ubunge uliocheleweshwa mnamo mwezi Machi na Aprili uliokipa ushindi chama cha Keita.

Kiongozi wa muungano wa upinzani Mali-Mahmoud DickoPicha: DW/K. Gänsler

Katika taarifa hapo jana, taasisi inayofanya tathmini ya elimu ya usalama ilionya kuwa  kuna chuki mbaya dhidi ya rais huku wengine wakiwaona viongozi hao kama wanaolinda maslahi yao finyu.Taasisi hiyo ilisema kuwa mikakati ya kutafuta suluhisho inafaa kuzingatia haja ya kuimarisha maisha ya kila siku ya raia wa Mali.

Mzozo nchini humo unayatia kiwewe mataifa jirani na washirika wa Mali wanaohofia kuwa taifa hilo lililoghubikwa na uasi kutoka kwa makundi ya itikadi kali huenda likatumbukia kwenye ghasia .Mkutano huo wa kilele unakuja baada ya kumalizika kwa mkutano wa ujumbe wa upatanishi kutoka Jumuiya ya Uchumi wa mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS), ambao ulimalizika siku ya Jumapili bila kupatanisha pande hizo mbili. Viongozi hao wa mataifa ya Afrika Magharibi watazingatia suluhu zilizopendekezwa katika mazungumzo ya faragha na rais wa Keita na upande wa upinzani wiki hii.

Juhudi hizo za upatanishi zinakuja baada ya wiki kadhaa za maandamano ya ghasia ambapo mamia ya watu waliuawa.Maelfu ya wafuasi wa upinzani wanamshtumu Keita kwa udhalilishaji wa kiasi kikubwa.Hali ya kukosa uthabiti wa kisiasa nchini Mali inaonekana kama tukio baya kwa eneo zima la Sahel ambalo tayari linakabiliwa na vitisho  vinavyoendelea kutoka kwa makundi kadhaa ya kigaidi na yanayotaka kujitenga.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW