1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za kuuzima moto Mlima Kilimanjaro zaendelea

12 Oktoba 2020

Wazima moto nchini Tanzania wanapambana kujaribu kuudhibiti moto unaouteketeza mlima mrefu zaidi barani Afrika, mlima Kilimanjaro. Kulingana na shirika la mbuga za kitaifa Tanzania TANAPA moto huo ulianza Jumapili.

Tansania Feuer auf dem Kilimandscharo
Picha: DW/Veronica Natalis

"Moto huo bado unaendelea na wazima moto kutoka TANAPA, taasisi zengine za serikali na wakaazi wa eneo hilo wanaendelea na juhudi za kuudhibiti moto huo," alisema Pascal Shelutete afisa wa TANAPA. Shelutete hakutoa taarifa zaidi.

Hapo Jumapili Shirika hilo la mbuga za kitaifa lilichapisha picha ambayo haionekani vizuri kwenye mtandao wa Twitter ikisema ni moto unaouteketeza mlima Kilimanjaro.

Mlima Kilimanjaro una urefu wa mita 6,000 sawa na futi 20,000 kutoka usawa wa bahari. Karibu watalii 50,000 wanaukwea mlima huo kila mwaka.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW