1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Asili na mazingiraPapua New Guinea

Uokoaji wasitishwa eneo la maporomoko Papua New Guinea

5 Juni 2024

Jeshi Papua New Guinea limesema leo kuwa miili ya mamia ya wanakijiji wa jamii moja ndogo jimboni Enga inayohofiwa kuzikwa katika maporomoko ya ardhi haitafukuliwa, likielezea shughuli za uokoaji kuwa "hatari sana".

Papua Guinea Mpya | Maporomoko ya ardhi huko Papua New Guinea
Wanakijiji wakitafuta manusura wa maporomoko ya ardhi katika kijiji cha Yambali, Nyanda za Juu za Papua New Guinea, Mei 27,Picha: Juho Valta/UNDP/AP/picture alliance

Meja Joe Aku, mmoja wa maafisa wakuu wa kijeshi wanaosimamia eneo hilo la mkasa, ameliambia shirika la habari la  AFP kwamba juhudi zote za kupata miili hiyo zimesitishwa kwa sababu ya hatari hiyo na kuonya kutokea kwa maporomoko zaidi ya ardhi. Aku, ameongeza kuwa eneo hilo litafungwa kwa muda usiojulikana. Serikali ya Papua New Guineainakadiria watu 2,000 wanaweza kuwa wamezikwa katika maporomoko hayo ya urefu wa mita 600, lakini kulingana na Aku, idadi hiyo inaweza kuwa takribani 650 huku mamlaka ya afya katika eneo hilo ikisema juhudi za muda za uokoaji ziliwezesha kupatikana kwa miili tisa tu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW