1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi zakuwepo na uchaguzi tulivu nchini Kenya

Wakio Mbogho23 Machi 2022

Tume ya uwiano na utangamano nchini Kenya imeorodhesha maeneo zaidi yenye uwezekano wa kuzuka ghasia za baada ya uchaguzi mkuu unaopangwa kufanyika Agosti mwaka huu.

Kenia Wahlwiederholung |  Unabhängige Wahlkommission (IEBC)
Picha: Reuters/T. Mukoya

Tume ya uwiano na utangamano nchini, NCIC, imefanya mikutano kutathmini vyanzo ya ghasia za baada ya uchaguzi mkuu katika maeneo ya Nyanza, Magharibi na Kaskazini Mashariki mwa nchi. Tume hiyo imetangaza maeneo matano yalioko kwenye kaunti za Kisumu na Kericho yanayofaa kuangaziwa kabla uchaguzi mkuu wa Agosti kufanyika. Gillian Nyambu, ni naibu mkurugenzi kwenye tume hiyo.

Kericho ni eneo linalotambulika kwa utajiri wake wa kilimo hasa kilimo cha majani chai ambayo huuza kwenye soko la kimataifa, na ni kati ya bidhaa za kuuzwa nje zinazotegemewa kwa uchumi wa nchi. Sekta hii imewavutia watu kutoka jamii tofauti wanaokuja hapa kufanya kazi kwenye mashamba na viwanda vya chai. Hata hivyo, historia ya uchaguzi eneo hili imekuwa ya kusikitisha kwani kila wakati wa kipindi cha uchaguzi, vurugu huzuka kati ya wenyeji na wageni.

Somia pia→Tume ya uchaguzi Kenya yapendekeza mabadiliko.

Kampeni ya amani kwenye mitandao ya kijamii

Tume ya uwiano imechukua mwelekeo wa kuwahusisha wanasiasa na viongozi wa kidini Picha: AFP/T. Karumba

Ili kuikabili hali, Tume ya NCIC imefanya mikutano na wadau kutoka sekta mbalimbali ikiwemo viongozi wa kidini, maafisa wa usalama, wataalam na wanasiasa kujadili ushirikiano katika kuangazia

Aidha tume hiyo inaendesha kampeni ya amani kwenye mitandao ya kijamii kupitia hashtag #Elections bila noma, ili kuwashawishi hasa vijana kukumbatia amani na maendeleo na kukataa kutumika kwa manufaa ya wanasiasa.

Gavana wa Kericho Paul Chepkwony ni kati ya wanasiasa wanaowarai wafuasi wao kudumisha amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Soma pia→Ruto aitaka tume ya IEBC kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru

Askofu wa jimbo katoliki la Kericho, Alfred Rotich amewataka wanasiasa kubadili mkondo wa siasa unaoshuhudiwa nchini, akiutaja kama mwelekeo unaotishia amani ya taifa.

Kwa sasa, tume hiyo inaendelea na mchakato wa kubaini maeneo yanayoathiriwa sana na matukio ya vurugu kaskazini mashariki mwa taifa, washiriki wakihusishwa katika kuunda mikakati ya kuikabili hali na kuhakikisha uchaguzi usiokuwa na ghasia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW