1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jukumu la makampuni ya kibinafsi katika kupiga vita umaskini duniani

Helle Jeppesen / Maja Dreyer17 Februari 2006

Mkutano wa kimataifa juu ya wajibu wa jamii na jukumu la makampuni ya kibinafsi katika kupiga vita umaskini duniani unaendelea huko Ureno. Wafadhili na wafanyibiashara wa kibinafsi wanaombwa mara kwa mara kuweka vitega uchumi katika miradi ya nchi zinazoendelea.

Hata hivyo wafadhili na wafanyibiashara wa kibinafsi wanaogopa hatari ya kiuchumi licha ya kuwepo uwezekano wa kupata faida za juu. Kufuatia hali hiyo benki za maendeleo kama vile shirika la Kijerumani la Maendeleo, kwa ufupi DEG, zimejitolea kuwasaidia wafanyibiashara hawa.

Kueneza shughuli za kiuchumi katika nchi za nje si kitu tu kinacholeta faida, bali pia ni hatua ya lazima ikiwa biashara iendelee. Bado lakini wafadhili wanaogopa kuingia katika masoko ýa nchi zinazoendelea - hata ikiwa matarajio ya kibiashara ni mazuri. Kwani katika kutoa vitega uchumi benki pia zinategemea maoni ya wale walioweka fedha zao kwenye benki ili kusiweko ya hatari yoyote.

Basi ni ukosefu hama huo ambao unasawazishwa na shirika la kifadhili la serikali ya Ujerumani kama DEG, shirika la kijerumani la maendeleo, kama msemaji wake, Winfried Polte, anavyoeleza: “Hilo ndilo jukumu letu. Kama kuna miradi, ambayo inaweza kugharamiwa na benki ya kibinafsi, sisi hatuhusiki. Badala yake tunaangalia nchi na miradi ambayo haipati wafadhili wa kibinafsi kwa sababu ya hatari za kiuchumi. Juu ya hayo, benki za kibinafsi kawaida zinakubali kukopesha fedha kwa miaka michache tu, lakini katika miradi mikubwa inabidi kutafuta fedha kwa ajili ya miaka mingi. Huko sasa tunahakikisha fedha kwa kipindi kirefu.”

Miradi inayosaidiwa na makopo ni ile tu yenye nia ya kuiendeleza nchi. Siyo bila sababu kwamba shirika la DEG ni shirika la kiserikali. Mara nyingi miradi inachaguliwa kwa kushirikiana na wizara ya mambo ya maendeleo ya Ujerumani. Vigezo vikuu ni: matarajio mazuri ya kiuchumi, kushirikiana na wafadhili wa kibinafsi pamoja na faida kwa jamii na kuhifadhi mazingira. Orodha ya vigezo kweli ni ndevu. Kwa upande mwingine, makubaliano ya benki kama DEG au mashirika mengine ya kimataifa yanayogharamia miradi yanaonekana kuwa ni ushahidi wa ubora wa mradi fulani.

Huo ni uzoefu wa Mohamed Ibrahim ambaye alianzisha na anaongoza shirika la simu za mkononi la Kiafrika, Celtel: “Benki hizi za maendeleo zinaweza kusaidia kuwavutia wafadhili wa kibinafsi, kwa sababu zinazijua nchi na hali zao. Mfadhili wa kibinafsi ni mtu mwoga ambaye hataki kujiweka hatarini. Kwa hivyo ni lazima mashirika ya kimataifa yajihusishe katika miradi hii. Hivyo tu ndipo fedha zitakwenda Afrika, na hivyo tu tunaweza kuona mabadiliko makubwa.”

Celtel ni moja ya kampuni zilizonufaika kwa kushirikiana na benki za maendeleo za kimataifa. Leo kampuni hiyo iliyoanzishwa mwaka 1998, ni moja ya kampuni zinazofaulu zaidi kiuchumi kwenye bara la Afrika. Mitandao yao ya simu za mkononi tayari imeendea katika nchi 14 za Afrika. Kwa upande wa shirika la DEG Celtel ni moja ya miradi mizuri kabisa, ingawa kwanza liliogopa kuingiza fedha nyingi.

Bara la Afrika kwa kawaida lina shida kubwa zaidi kuwavutia wafadhili kutoka nje. Bara la Marekani ya Kusini wakati huo huo linaangaliwa kutokuwa na hatari tena, na huko Asia wafadhili wanauona uwezekano mkubwa wa kiuchumi. Ikiwa wawekeze uchumi barani Afrika lakini, wengi hata hawafikiri, moja kwa moja wanakataa. Kwa sababu hiyo shirika la DEG liliongeza bidii zake katika nchi za Kiafrika kwa kushirikiana na mashirika mengine yanayotoa mikopo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW