1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Usalama wa chakulaTanzania

Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika lahitimishwa Tanzania

Florence Majani8 Septemba 2023

Wakati Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika likihitimishwa, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na wadau wa kilimo, watafiti na wanasayansi, wametoa ushauri juu ya namna ya kuboresha sekta hiyo.

Symbolbild China in Afrika | Tansania
Picha: Li Sibo/Photoshot/picture alliance

Jukwaa la Mfumo wa Chakula Afrika(AGRF) linahitimishwa leo jijini hapa huku wadau mbalimbali waliohudhudhuria mkutano huo wakishauri na kutoa mbinu za kuiboresha sekta ya kilimo na chakula.

Akizungumza jana katika siku ya nne ya jukwaa hilo, lililojumuisha wadau wa kilimo zaidi ya 4000, Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali iliweka mkakati wa kuhakikisha sekta ya kilimo inachangia asilimia 10 kwenye pato la taifa ifikapo 2030 na jitihada hizo zinaendelea.

Rais Samia amesema katika kutekeleza azma hiyo, serikali inawekeza katika kushirikisha vijana na wanawake katika biashara za kilimo, huku ikitenga Tsh 10 bilioni kutoa mikopo kwa ajili ya kilimo biashara.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu HassanPicha: Presidential Press Service Tanzania

Wadau wengine katika jukwaa hili, wameshauri masuala ya kuyawekea mkazo ili kuhakikisha kuna upatikanaji wa uhakika wa chakula barani Afrika. Dr Oforo Kimambo Mtaalamu wa Hali ya Hewa kutoka Chuo cha Kilimo(SUA), ameshauri mambo kadhaa ili Afrika ifikie kiwango cha juu cha upatikanaji wa chakula.

Wadau katika Jukwaa hili ambalo leo litahitimishwa na Naibu Waziri Mkuu, Dk Dotto Bitteko, wanatarajia kujadili maazimio ya nchi katika sekta za kilimo, kuonyesha manufaa ya uwekezaji katika sekta hiyo, mustakabali wa usalama wa chakula kuelekea 2030 na vidokezo vya muhimu kwa mkutano mkuu wa mazingira wa COP 28 unaofanyika Novemba mwaka 2023 huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Jukwaa la mfumo wa chakula lilianza Septemba 5 na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo ili kujadili na kuchukua hatua za kiutendaji katika kiboresha upatikanaji na usalama wa chakula Afrika.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW