1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Julai ya 2023 ni mwezi uliokuwa na joto zaidi duniani

8 Agosti 2023

Ripoti mpya ya uchunguzi wa mabadiliko ya hali ya hewa barani Ulaya inaonesha kuwa Julai ulikuwa mwezi wenye kiwango cha juu zaidi cha joto kilichowahi kurekodiwa katika uso wa dunia.

Portugal Waldbrände
Picha: PATRICIA DE MELO MOREIRA/AFP

Kwa rekodi hii mpya, mwezi Julai ulikuwa na fukuto la joto kali iliyoambatana na majanga ya moto kutokana na ongezeko la joto la nyuzi joto 0.33, zaidi ya  kile kilichorekodiwa Julai, 2019 cha wastani wa nyuzi joto 16.63. Mwezi huo ulikuwa na ongezeko la joto la nyuzi joto 0.72 zaidi ya ule wastani uliorekodiwa katika kipindi kama hicho cha Julai kwa miaka ya 1991 hadi  2020.

Hili ongezeko la sasa la nyuzi joto 1.2 ulimwenguni, ambalo limekuwa likipanda tangu mwishoni mwa miaka ya 1800, kimsingi limetokana na matumzi ya nishati ya mafuta, hali joto kuongezeka zaidi, kwa kipindi kirefu na kuzidisha hali mbaya ya hewa kama vimbunga na majanga.

Kupanda kwa joto katika maeneo ya bahari.

Kikosi cha kuzima moto kikiwa kazini kuzima moto wa nyika katikati mwa taifa la UrenoPicha: PATRICIA DE MELO MOREIRA/AFP

Kwa mujibu wa takwimu za uchuguzi huo wa Ulaya kiwango cha joto katika eneo la uso wa bahari lilipanda hadi nyuzi joto 20.96 Julai 30. Rekodi za awali za Machi 2016, za asasi yenye kufuatilia mabadiliko ya tabia nchi (CCCS) ilionesha kiwango cha nyuzi joto 20.95. Carlo Buontempo ni mkurugenzi wa shirika hilo anamesema "Tunaweza kusema kwamba sio tu wiki ya kwanza ya Julai iliyokuwa na joto zaidi katika rekodi, lakini wiki tatu za Julai zilikuwa zenye joto zaidi. Kutokana na matokeo hayo tunaweza kusema kwamba hadi mwishoni mwa mwezi Julai, tumepata na rekodi ya Julai yenye joto kali zaidi."

Ripoti hii ya uchuguzi wa hali ya hewa ya Umoja wa Ulaya inasema mawimbi ya joto yameshuhuduwa katika maeneo mengi ya kaskazini mwa dunia, likiwemo la kusini mwa Ulaya, Joto lililo juu ya wastani limeshuhudiwa katika nchi kadhaa za Amerika ya Kusini na karibu zaidi na Antaktik.

Onyo la wanasayansi kuhusu joto la dunia.

Wasayansi walikwisha toa onyo la mapema kuwa mwezi Julai utakuwa wa kuvunja rekodi ya joto. Maeneo ya bahari kuu ya ulimwengu pia yaliweka rekodi ya kiwango kipya cha joto, hali iliyozusha wasiwasi kuwepo kwa athari mbaya ya hali ya hewa itayaoiathiri dunia, viumbe vya baharini na jamii ya watu wanaoishi katika maeneo ya pwani.

Dunia kwa wakati huu ipo katika hatua za awali za tukio la El Nino, linalotokana na maji yenye joto lisilo la kawaida katika eneo la mashariki mwa Pasifiki. El Nino kwa kawaida hutoa halijoto duniani kote, ikiongezeka maradufu kutokana na ongezeko la joto linalotokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na uhrabifu wa mazingira utokanao na binadamu.

Soma zaidi:Joto kali lasababisha maafa ya moto kwenye nchi kadhaa Ulaya

Wanasayansi wanaamini kwamba mwaka  2023 au 2024 mmoja kati ya hiyo itamalizika kwa kuwa  mwaka wenye joto zaidi na kuvinja rekodi ya mwaka 2016.

Chanzo: AFP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW