Assange akubaliwa kupinga hukumu ya kuhamishwa Marekani
20 Mei 2024Muasisi wa tovuti ya kuvujisha nyaraka za siri Wikileaks Julian Assange ameshinda nafasi ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama moja ya Uingereza iliyoidhinisha apelekwe Marekani kusikiliza kesi yake dhidi ya Uvunjifu wa sheria ya usalama wa kitaifa.
Majaji wawili wa mahaka ya juu mjini London walimpa Assange nafasi ya kukata rufaa baada ya awali kuitaka Marekani ithibitishe kutoa hakikisho la kulinda uhuru wa kujieleza katika kesi yoyote inayohusu taifa hilo.
Soma pia: Biden asema anatafakari ombi la Australia la kuifuta kesi dhidi ya muasisi wa Wikileaks Assange
Assange aliye na miaka 52 hakuwepo mahakamani wakati uamuzi huo ulipotolewa.
Jullian Assange anatuhumiwa kuchapisha nyaraka nyingi za siri za Marekani. Kwa miaka mingi, Australia imekuwa ikiitolea wito Marekani kuitupilia mbali kesi yake dhidi ya Assange, raia wa Australia ambaye anapinga juhudi za Marekani kutaka ahamishiwe nchini humo kutoka gereza la Uingereza.