1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumbe za Kimarekani kuizuru Korea ya Kaskazini

3 Januari 2004
WASHINGTON: Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa huenda jumbe mbili za Kimarekani hapo wiki ijayo zitaizuru Korea ya Kaskazini. Hata hivyo jumbe hizo haziendi Korea ya Kaskazini kwa niaba ya serikali, alisema msemaji wa Wizara hiyo. Halmashauri ya Siasa ya Nje katika Baraza la Senate la Marekani imeeleza kuwa washauri wake wawili wana mipango ya kwenda Jumamosi ya leo Korea ya Kaskazini. Kuna uwezekano kuwa wajumbe hao wawili wataruhusiwa kuitembelea miradi ya kinyuklea ya nchi hiyo huko Yongbyon. Ujumbe wa pili wa kibinafsi utakuwa ule wa mabingwa, akiwemo pia mtaalamu mmoja wa kinyuklea. Wanachama wa ujumbe huo waliliambia gazetila USA TODAY, Korea ya Kaskazini imeahidi kuwaruhusu mabingwa wao kukizuru kinu cha kinyuklea cha Yongbyon. Marekani inaitilia shaka Korea ya Kaskazini kutaka kuunda silaha za kinyuklea.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW