Jumuiya NATO yaongeza uwepo wake eneo la Arctic
11 Februari 2026
Hii ni kufuatia mzozo kuhusiana na kisiwa cha Greenlandkusababisha mpasuko kati ya Marekani na washirika wake wa Ulaya.
Kulingana na Kamanda wa Ulaya Alexus Grynkewich, mpango huo ujulikanao kama Arctic Sentry utatumia nguvu ya NATO kuhakikisha eneo hilo linasalia kuwa salama.
Kuongeza uwepo wa NATO huko Greenland ni jambo lililopendekezwa na baadhi ya mataifa ya Ulaya ili kupunguza mzozo kukihusu kisiwa hicho, ambacho Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kukitwaa akisema asipofanya hivyo, basi Urusi au China ndio watakaokiteka.
Baada ya mkutano na Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte katika Jukwaa la Kiuchumi Duniani lililofanyika huko Davos, Uswisi mwezi uliopita wa Januari, Trump alitangaza kuwa tayari kuna rasimu ya makubaliano ya baadae kuhusu Greenland na eneo zima la Arctic.