1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya ya Afrika Mashariki yapitisha bajeti yake

Yusra Buwayhid
29 Juni 2021

Jumuiya ya Afrika Mashariki imepitisha bajeti ya dola milioni 91.7 kwa mwaka wa fedha 2021-2022.

Logo Ostafrikanische Gemeinschaft EAC

Bajeti hiyo imetaja vipaumbele 10 ikiwepo maendeleo ya sekta binafsi, ulinzi na usalama pamoja na janga la virusii vya corona kwa nchi zote wanachama. 

Akisoma hotuba ya bajeti hiyo kwa niaba ya mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, katibu tawala wa Jumuiya hiyo Ken Obura, amesema bajeti hiyo inapitishwa kipindi ambacho janga la virusi vya corona limeuvuruga vibaya uchumi wa jumuiya hiyo kongwe barani Afrika. 

Bajeti ya mwaka huu imepungua ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha uliopita ambayo ilikuwa dola zaidi ya 97 za Kimarekani. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW