1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Jumuiya ya ASEAN haiutambui uchaguzi wa Myanmar

30 Januari 2026

Jumuiya ya ushirikiano ya Kusini-Mashariki mwa Asia, ASEAN imesema haiutambui uchaguzi uliofanyika hivi karibuni nchini Myanmar, ambao ni wa kwanza tangu jeshi liliponyakua mamlaka mnamo 2021.

Malaysia Kuala Lumpur 2025 | Theresa Lazaro akiwa kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya ASEAN
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufilipino Theresa Lazaro akihudhuria Kongamano la 32 la Jumuiya ya Mataifa ya Kusini-Mashariki mwa Asia (ASEAN) wakati wa mkutano wa 58 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa ASEAN Kuala Lumpur Julai 11, 2025.Picha: Mohd Rasfan/AFP/Getty Images

Jumuiya hiyo yenye wanachama 11 ikiwa ni pamoja na Myanmar aidha ilikataa kuitambua serikali ya kijeshi ya taifa hilo tangu jeshi lilipochukua mamlaka kwa nguvu kutoka kwa serikali iliyochaguliwa ya Aung San Suu Kyi mnamo 2021 na kuitumbukiza nchi hiyo vitani.

Hatua hiyo iliyothibitishwa na waziri wa mambo ya Nje wa Ufilipino Theresa Lazaro inachukuliwa kuwa pigo kubwa kwa juhudi za watawala wa kijeshi wa Myanmar kutambuliwa kimataifa.

Lazaro aliyekuwa akizungumza baada ya kuongoza mkutano wa kwanza mkubwa wa mawaziri kwa mwaka huu hakueleza ikiwa jumuiya hiyo itakuja kubadilisha msimamo wake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW