1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya ya Kimataifa yaahidi kuiunga mkono Syria

14 Februari 2025

Mataifa ya magharibi na yale ya ulimwengu wa kiarabu yameahidi kuiunga mkono Syria katika kipindi muhimu cha mpito kinachoendelea baada ya kuangushwa utawala wa Rais Bashar al-Assad.

 Rais wa Mpito wa Syria Ahmed al-Sharaa
Rais wa Mpito wa Syria Ahmed al-Sharaa.Picha: Syrian Presidency/Handout via REUTERS

Ahadi hiyo imetolewa mwishoni mwa mkutano wa mjini Paris ulioyaleta pamoja mataifa 20 kujadili kuipiga jeki Syria wakati taifa hilo linaunda upya taasisi na mifumo ya utawala.

Viongozi kutoka nchi za magharibi na kiarabu ikiwemo Uturuki, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Canada na Japan wamekubaliana kufanya kazi pamoja kuhakikisha kipindi cha mpito nchini Syria kinakuwa cha mafanikio.

Tamko lao la pamoja limesema linauunga mkono utawala mpya wa Syria kwenye kupambana dhidi ya vitendo vyote vya kigaidi na itikadi kali. Mkutano huo pia umetoa mwito wa kila kundi nchini humo kujumuishwa kwenye mchakato wa kuunda upya taasisi za utawala.

Syria hivi sasa inaongozwa na Rais wa Mpito Ahmed al-Sharaa aliyeoongoza kundi la waasi kuuangusha utawala wa Assad mwezi Disemba mwaka jana. Kiongozi huyo ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa kwamba atalinda haki za makundi ya wachache.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW