SiasaSamoa
Ghana yashika nafasi ya kuongoza Jumuiya ya Madola
26 Oktoba 2024Matangazo
Mataifa hayo yameteua katibu mkuu huyo mpya katika mkutano wa kilele, nchini Samoa siku ya Ijumaa.
Botchwey alikuwa mmoja wa wagombea watatu wa nafasi hiyo, miongoni mwa wengine ambao kwa ujumla waliunga mkono miito kwamba mataifa ya Ulaya yanatakiwa kushughulikia madhila yaliyosababishwa na ukoloni na utumwa.
Mbunge huyo wa zamani, amekuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka saba, akiiongoza Ghana katika kipindi cha miaka miwili kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichomalizika mwaka 2023.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola anaweza kushika nafasi hiyo kwa awamu mbili, za miaka minne.