KABUL: 9 wauliwa katika mashambuliano
12 Januari 2004Matangazo
Takriban watu 9 wameuawa katika matukio tafauti ya mapigano kusini mwa Afghanistan, ambako maafisa wanataja kuwa askari 5 ni miongoni mwa waliouawa. Imearifiwa pia kuwa watu wengine 3 wamejeruhiwa katika mapigano ya walanguzi wa madawa ya kulevya katika jimbo la kusini la Kandahar. Katika tukio lingine, imeripotiwa kuwa wapiganaji 4 wanaokisiwa kuwa wafuasi wa Taliban wameuawa na majeshi ya serikali baada ya kujaribu kuzika mabomu ya kutegwa ardhini.
