Kabul. Afghanistan kuitambua Israel baada ya taifa la Palestina.
16 Oktoba 2005Matangazo
Msemaji wa rais wa Afghanistan amesema leo kuwa rais wa nchi hiyo Bwana Hamid Karzai ataitambua serikali ya Israel iwapo taifa huru la Palestina litaundwa. Afghanistan ambayo ni nchi ya Kiislamu haijakuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Israel.
Karzai ameongeza kuwa Israel itabidi kuheshimu uhalali wa kuwapo taifa la Palestina kabla ya Afghanistan kuanza kujenga mahusiano na Israel.
Ametoa maelezo hayo wakati wa mahojiano na waandishi wa habari wa Israel mjini Kabul mwezi huu, Karim Rahimi msemaji wa rais ameliambia shirika la habari la Reuters.
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Israel Mark Regev ameukaribisha uwezekano wa kuboreshwa kwa uhusiano na Afghanistan.