Kabul. Kundi la rais lapata ushindi.
14 Novemba 2005Matangazo
Nchini Afghanistan , waangalizi wa uchaguzi wamesema kuwa waungaji mkono wa rais Hamid karzai wamepata ushindi katika uchaguzi wa bunge.
Kundi la Karzai limeshinda asilimia 60 ya kura katika bunge jipya , kwa mujibu wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.
Maafisa wanaosimamia uchaguzi wamesema karibu nusu ya viti 249 vimekwenda kwa viongozi wa kiukoo na viongozi wa makundi ya wapiganaji wa zamani, pamoja na wanachama wa utawala wa zamani wa Taliban. Matokeo ya uchaguzi yalitangazwa siku ya Jumamosi karibu miezi miwili baada ya uchaguzi kutokana na madai kadha ya wizi wa kura ambayo yalibidi kuthibitishwa.