1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Majadiliano kuachilia huru mateka wa Korea ya Kusini

22 Julai 2007

Ripoti zinasema,vikosi vya usalama vya Afghanistan,vimezingira eneo ambako wanamgambo wa Taliban wamewazuia mateka 23 wa Korea ya Kusini. Lakini operesheni ya kijeshi,kuwaokoa mateka hao bado haikuanza,kwani kunafanywa majadiliano ya kuwaachilia huru mahabusu hao wa Korea ya Kusini.

Wakati huo huo,Korea ya Kusini imethibitisha kuwa inafanya matayarisho ya kuondosha vikosi vyake kutoka Afghanistan,ifikapo mwisho wa mwaka huu, kama ilivyopangwa tangu hapo awali.Mipango hiyo haikuathiriwa na utekaji nyara huu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW