1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Mgombea mwengine wa uchaguzi auwawa

17 Septemba 2005

Mgombea mwengine wa uchaguzi nchini Afghanistan ameuwawa ikiwa ni siku mbili tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa bunge ambao ni wa kwanza kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miongo kadhaa.

Waasi wa Taliban wamesema wamempiga risasi na kumuuwa Abdul Hadi hapo Alhamisi jioni baada ya kumburuza kutoka nyumbani kwake.Takriban watu milioni 12 na nusu wana haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa hapo kesho.Zaidi ya wagombea 5,700 wanawania viti 249 bungeni pamoja na nafasi kwenye mabaraza ya miji.

Zaidi ya wanajeshi wa kigeni 30,000 na wanajeshi wenyeji wa nchi hiyo 100,000 watapiga doria kwenye vituo vya kupiga kura.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW