1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wanajeshi sita wa Canada wauwawa

5 Julai 2007

Canada imetangaza kwamba wanajeshi wake sita waliokuwa katika kikosi cha kulinda amani cha jumuiya ya kujihami ya kambi ya magharibi NATO nchini Afghansitan wameuwawa pamoja na mkalimani wao.

Wanajeshi hao waliuwawa wakati gari lao lilipokanyaga bomu lililokuwa limetagwa kando ya barabara na kulipuka kusini mwa Afghanistan.

Wanamgambo wa kundi la Taliban wametangaza kuhusika na shambulio hilo lililoelezwa kuwa baya zaidi kuwahi kufanywa tangu mwezi Aprili mwaka huu, wakati wanajeshi wengine wa Canada walipouwawa kwenye shambulio kama hilo.

Wanajeshi 105 wa kigeni wameuwawa nchini Afghanistan mwaka huu, wengi wakiwa katika operesheni mbalimbali nchini humo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW