Kabul. Wanajeshi wawili wa Afghanistan wauwawa mmoja wa NATO ajeruhiwa.
16 Desemba 2006Matangazo
Mtu mmoja aliyejitoa muhanga ambaye alivaa baibui la kike amejeruhi wanajeshi wawili wa Afghanistan katika shambulio katika jimbo la Paktia. Mtu wa pili kujitoa mhanga alilipua bomu katika gari karibu na magari ya deraya ya jeshi la NATO katika jimbo hilo la Paktia, na kuuwa wanajeshi wawili wa Afghanistan na kumjeruhi mwanajeshi mmoja wa jeshi la NATO.
Wakati huo huo , majeshi ya NATO yanayoongozwa na Uingereza yanaendesha kampeni kubwa katika jimbo la kusini la Kandahar, eneo ambalo linadhibitiwa na wapiganaji wa Taliban. Mamia ya wanajeshi wa Uingereza, Estonia na Denmark wakisaidiwa na idadi kadha ya magari ya deraya yameondoka kutoka katika jimbo la Helmand na kwenda katika jimbo la jirani la Kandahar.