KABUL: Wataliban walipua askari 5
29 Desemba 2003Matangazo
Takriban maafisa 5 wa usalama wa serikali ya Afghanistan wameuawa katika mlipuko wa bomu unaodhaniwa kuwa shambulio la kujitolea mhanga. Tukio hilo limefanyika karibu na uwanja wa ndege wa mjini Kabul wakati mtu aliyekisiwa kufanya hujuma hiyo alipokamatwa na maafisa wa idara ya upelelezi. Mtu huyo alifaulu hata hivyo kujilipua na mabomu aliyokuwa nayo mwilini. Wapiganaji wa utawala wa zamani wa Taliban, uliopinduliwa mwaka jana kwa msaada wa askari wa Marekani wamejigamba kuwa wamehusika katika shambulio hilo.
