1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL Wateka nyara wamweka kiporo mfaransa wanaemshikilia

5 Mei 2007

Mataliban wanaomshikilia mfaransa waliomteka nyara pamoja na raia watatu wa Afghanistan wameipa Ufaransa muda zaidi.

Wateka nyara hao wamesema wataamua kitakachotokea kwa mfaransa huyo na wenzake baada ya matokeo ya uchaguzi wa rais kufahamika nchini Ufaransa hapo kesho.

Mfaransa huyo alitekwa nyara mwanzoni mwa mwezi aprili pamoja na raia hao watatu wa Afghanistan.

Wateka nyara hao wametishia kumwuua mfaransa huyo na wenzake ikiwa Ufaransa haitaondoa majeshi yake kutoka Afghanistan.