KABUL:Askari saba wauwawa
25 Aprili 2007Matangazo
Bomu lililotegwa kandoni mwa barabara limelipuka na kuwauwa askari saba katika eneo la mpaka wa Afghanistan na Pakistan.
Maafisa wa Afghanistan wamesema kwamba askari hao waliouwawa walikuwa katika msafara wa magari kumi katika mkoa wa Pakita wakati walipopata ajali hiyo.
Hakuna mtu au kundi lolote lililodai kuhusika na shambulio hilo.