1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa auwawa

17 Novemba 2003
Mwanamke mmoja wa Kifaransa anayefanya kazi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR amepigwa risasi na kuuwawa hapo jana katika mji wa Ghazni nchini Afghanistan. Hayo ni mauaji ya kwanza ya mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan tokea kuangushwa kwa utawala wa Taliban na vikosi vilivyoongozwa na Marekani miaka miwili iliopita. Maafisa wa serikali za mitaa katika mji huo wamewakamata watu wawili wenye silaha. Wamesema wanaamini wauaji walikuwa ni waasi kutoka utawala uliopinduliwa wa Taliban ambao umerudi kufanya mashambulizi kwa baadhi ya sehemu za nchi hiyo katika miezi ya hivi karibuni.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW