1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Mgombea mmoja wa mwanamke ajeruhiwa na watu waliokuwa na silaha.

15 Septemba 2005

Kuelekea uchaguzi siku ya Jumapili nchini Afghanistan,mgombea mmoja mwanamke amejeruhiwa na watu waliokuwa na silaha katika jimbo la Nuristani.

Gavana wa jimbo hilo,amesema hakuna mtuhumiwa yeyote aliyekwishakamatwa kutokana na shambulio hilo.

Kikundi cha kutetea haki za binadamu cha Human Rights watch,kimetoa taarifa inayoeleza kuwa mashambulio yanayofanywa wakati huu kueleka siku ya uchaguzi,yanajenga hofu miongoni mwa wagombea na wapiga kura.Hata hivyo kikundi hicho kimeeleza maandalizi kwa ajili ya uchaguzi huo yanakwenda vizuri.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afghanistan Ali Ahman Jalali,amesema wapiganaji wa kikundi cha Taliban,wanajaribu kudhoofisha shughuli za uchaguzi wa siku ya Jumapili,lakini akaongeza hawatafanikiwa.

Waziri Jalali amesema zaidi ya wanajeshi 100,000 wakisaidiana na askari polisi,wakiwemo wanajeshi wa vikosi vya kulianda amani vya NATO pamoja na wale wa Marekani,wamejizatiti kuweka ulinzi wa kutosha kuelekea siku ya uchaguzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW