Kaburi la pamoja lagunduliwa Darfur
13 Julai 2023Taarifa hiyo imetolewa na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ikisema kuwa inazo taarifa za kuaminika kwamba ni vikosi maalumu vya dharura (RSF) nchini Sudan vinahusika na mauaji hayo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa, wakaazi wa eneo hilo walilazimika kuitupa miili hiyo kwenye sehemu iliyo wazi.
Soma zaidi: HRW yasema mauaji ya kutisha yanatokea Darfur
Viongozi wa kikabila Darfur watangaza kuiunga mkono RSF
Miili ya wanawake na watoto ilikuwa miongoni mwa maiti hizo.
Kadhia hiyo ilitukia kati ya tarehe 20 na 21 mwezi uliopita karibu na mji mkuu wa Darfur, EL-Geneina.
Baadhi ya watu walifariki kutokana na majeraha ambayo hayakutibiwa baada ya wimbi la vurugu za vikosi vya dharura vya RSF na wanamgambo washirika, zilizotokea baada ya kuuawa kwa gavana wa eneo hilo.
Kamishna wa Haki za Binaadamu wa Umoja Mataifa, Volker Turk, amelaani vikali mauaji hayo.