1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kadinali Pell huru baada ya hukumu kufutwa

Saleh Mwanamilongo
7 Aprili 2020

Korti kuu ya Autralia imefuta hukumu ya miaka sita jela dhidi ya kadinali Pell aliekuwa akitumikia kifungo hicho kwa muda wa mwaka mmoja sasa.Pell amesema uamzi huo wa korti kuu umekomesha udhalimu mkubwa dhidi yake.

Kadinali George Pell wa kanisa katoliki achiliwa huru
Kadinali George Pell wa kanisa katoliki achiliwa huruPicha: picture-alliance/AP Photo/A. Brownbill

Kadinali George Pell wa kanisa katoliki nchini Autralia amechiliwa huru baada ya kesi yake kuhusu unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto. Koti kuu ya Autralia imefuta hukumu ya miaka sita jela dhidi ya kadinali huyo wa miaka 78 ambaye alikuwa akitumikia kifungo hicho kwa muda wa mwaka mmoja sasa. Kwenye taarifa baada ya kuachiwa kwake George Pell amesema kwamba uamzi huo wa koti kuu umekomesha udhalimu mkubwa dhidi yake.

Kwa kauli moja majaji saba wa koti kuu ya Australia wamehisi kwamba hukumu iliyotolewa kwenye koti ya rufaa ya Victoria haikuzingatia kuhusu uwezekano wa mashaka kuhusu kufanyika kwa makosa hayo. Kisheria mashaka yoyote ni kwa faida ya mtuhumiwa, wanaelezea majaji hao kwenye uamzi wa hivi leo. Kiongozi huyo wa kanisa aliyekuwa anashikilia nafasi ya mweka hazina Vatican, alikuwa miongoni mwa viongozi wenye nguvu zaidi kanisani.

Kadinali George Pell  alihukumiwa mwaka 2019 baada ya kukutwa na hatia ya unyayasaji wa vijana wawili mkwaka 1996, lakini alikana kuhusika. Katika uamzi wake mwaka uliopita, koti ya rufaa ilimkuta na hatia, ikiwemo ya kumuingilia mtoto chini ya miaka 16, na hatia zingine nne za kuwafanyia vitendo visivyo vya kawaida watoto wa chini ya umri wa miaka 16.

Papa Francis awaombea waliohukumiwa pasina kufanya makosaPicha: picture-alliance/IPA/CPP/Catican Media

Kwenye ibada ya asubuhi hii leo huko Vatican, saa chache baada ya kuachiwa kwake kadinali Gerorge Pell, papa Fancis aliwaombea wale waliohukumiwa pasina kufanya makosa.

''Nilitaka kuwaombea leo wale ambao wamesononeka na hukumu dhalimu ilikuwa ili kuwatesa. Msiwape maadui zangu uwezo kwa kutoa ushuhuda wa uongo dhidi yangu na kwa watu wanaotaka vurugu.''

Baba wa mmoja wa vijana waimbaji wa kanisa wakati huo ambao walimtuhumu kadinali Pell, amesema kwamba ataomba kulipwa fidia.

Lisa Flynn, wakili wa baba wa kijana huyo ambaye alifariki mwaka 2014, ameelezea kuchukizwa kwa mteja wake  na uamuzi huo wa mahakama kuu ya Ausrtalia hii leo. Na kuendelea kusema kwamba hana imani tena na mfumo wa kisheria wa nchi yake.

Kwa upande wake Cathy Kezelman, kiongozi wa shirika la kuunga mkono waathirika wa Blue Knot Foundation, amesema uamuzi huo wa koti kuu ni janga kwa waathirika wengi.

Kwa upande wake kadinali Pell amelezea kwamba hana chuki yoyote kwa waliomushitaki. Huku akiendelea kusema kuwa kesi yake siyo kura ya maoni dhidi ya kanisa katoliki.

Alipoachiwa huru hii leo, kadinali Pell alienda moja kwa moja kwenye nyumba ya kanisa ya Melbourne. Uamzi ulitolewa pasina ya yeye kuwepo kutokana na juhudi za viongozi wa Australia za kupambana na ugonjwa wa Corona.

Kanisa katoliki duniani kote kwa miaka ya hivi karibuni, limekumbwa na kashfa ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto, na kudaiwa kuwa wamekuwa wakificha masuala hayo. Kwa wakati wote kadinali Pell amekanusha kuhusika na matukio yote.

Papa Francis yupo katika wakati mgumu kuweza kuweka uongozi na kuzalisha suluhu itakayoleta muafaka juu ya mgogoro mkubwa unaolikumba kanisa, huku wengine wakisema limepoteza mamlaka yake ya kimaadili na kuwa katika hali mbaya.