1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kagame aapishwa, asema amani ya kanda ni 'kipaumbele' chake

12 Agosti 2024

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameapishwa jana Jumapili kwa muhula wa nne, akisema amani ya kikanda ndiyo kipaumbele, katikati mwa mzozo unaoendelea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Kigali, Rwanda| Kuaishwa kwa Paul Kagame
Rais Paul Kagame akihutubia wageni wakati akianza muhula mpya.Picha: Presidency Of Rwanda/Anadolu/picture alliance

Kagame alishinda uchaguzi wa mwezi uliyopita kwa asilimia 99.18 ya kura, na kumpa muhula mwingine wa miaka mitano madarakani.

Wakuu kadhaa wa mataifa na wageni wengine kutoka mataifa ya Afrika walijiunga kwenye sherehe hiyo ya uapisho iliyofanyika mjini Kigali.

Matokeo ya uchaguzi wa Julai 15 hayakuwa na mashaka yoyote kwa Kagame, ambaye amelitawala taifa hilo dogo kwa mkono wa chuma, tangu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, kama kiongozi wa nyuma ya pazia na kisha rais.

Soma pia:Paul Kagame: Shujaa au Dikteta? 

Kagame amesema amani ya kanda ndiyo kipaumbele cha Rwanda, lakini haiwezi kuletwa na yeyote au kutoka kokote hata wawe na nguvu kiasi gani, endapo upande unaohusika zaidi haujafanya kinachohitajika.

Rais wa Angola Joao Lounreco, akiwa miongoni mwa waliohudhuria sherehe ya Jumapili, alitarajiwa kufanya mazungumzo ya faragha na Kagame, kuhusu mpango wa kusitisha vita DRC uliofikiwa wiki iliyopita.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW