Rais wa Rwanda Paul Kagame amefanya ziara fupi nchini Uganda ambapo amefanya mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake rais Yoweri Museveni. Baada ya kikao hicho cha faragha, wawili hao walizungumzia mgogoro wa wakimbizi wa DRC na kuutaka Umoja wa Mataifa kushughulikia hali ya usalama inayozidi kuzoroto mashariki mwa nchi hiyo.