1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kagame atishia kuwakamata "wanaoabudu umasikini"

25 Agosti 2023

Rais Paul Kagame wa Rwanda ametishia kuwakamata waumini wa Kanisa Katoliki wanaotembelea maeneo ya kuhiji nchini humo, akiwatuhumu kwa kile alichokiita "kuabudu umaskini."

Ruanda l Präsident Paul Kagame
Picha: Dan Kitwood/POOLAFP

Kagame, ambaye yeye mwenyewe ni muumini wa Kanisa Katoliki, ameyasema haya wakati akizungumza katika mkutano mmoja wa vijana nchini Rwanda.

Kila mwaka, maelfu ya watu, wengi wao wakiwa wanasafiri kwa miguu kwa siku kadhaa, wanatembelea mji wa Kibeho ulioko kusini mwa Rwanda ambako Bikira Maria anadaiwa kuwatokea wasichana watatu wa shule miongo minne iliyopita.

Soma zaidi: Rwanda: Padri aliyegeukia siasa azuiwa Nairobi

Lakini akizungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP, msemaji wa serikali amekanusha kwamba Kagame alikuwa akiuzungumzia mji wa Kibeho, akidai huenda ikawa alikuwa anazungumzia eneo moja ambalo si maarufu sana magharibi mwa Rwanda.