Janga
Kagame na wenzake wakumbuka mauaji ya kimbari ya mwaka 1994
7 Aprili 2024Matangazo
Amesema mambo yaliyopelekea mauaji hayo kutokea hayatopewa nafasi tena ya kujitokeza katika siasa za Rwanda. Rais huyo wa Rwanda ameongeza kuwa siasa za Rwanda haziegemei misingi ya kikabila wala dini mambo yanayoaminika pia kuchochea mauaji hayo.
Kagame na mkewe waliwaongoza viongozi 37 waliofika katika eneo la kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari katika mji wa Kigali ambapo zaidi ya wahanga 250,000 wanaaminika kuzikwa huko.
Wanyarwanda wakumbuka miaka 30 ya mauaji ya kimbari
Zaidi ya siku 100 ya mauaji hayo yaliyoanza Aprili 7 mwaka wa 94, watutsi na wahutu waliojaribu kuwalinda waliuwawa kinyama na wahutu wenye msimamo mkali walioongozwa na jeshi la Rwanda na wanamgambo waliojulikana kama Interahamwe.