1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kais athibitishwa kushinda asilimia 90.7 Tunisia

12 Oktoba 2024

Tume ya Uchaguzi nchini Tunisia imemthibitisha rasmi Rais Kais Saied kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita, kwa kupata asilimia 90.7 ya kura.

Tunisia I Tunis uchaguzi
Rais Kais Saied wa Tunisia akiwapungia mkono wafuasi wake mjini Tunis.Picha: Anis Mili/AP/picture alliance

Matokeo hayo yaliyotangazwa jana, hayana tafauti kubwa na matokeo ya awali, ambayo yanampa fursa kiongozi huyo anayetawala kwa mkono wa chuma kutawala kwa muhula mwengine wa miaka mitano madarakani.

Vyama vya upinzani na makundi ya haki za binaadamu yamehoji uhalali wa matokeo hayo, ambayo yamepatikana baada ya wagombea waliokuwa madhubuti kuondoshwa kwenye uchaguzi wenyewe.

Soma zaidi: Rais wa Tunisia Kais Saied anatarajiwa kushinda muhula wa pili

Wagombea pekee walioruhusiwa kuwania walikuwa ni Ayachi Zammel, aliyetangazwa kupata asilimia 7.3 na Zouhair Maghzaoui aliyepata takribani asilimia 2.

Kwa ujumla, watu waliojitokeza kupiga kura walikuwa ni asilimia 28.8 tu ya wapiga kura wote halali.