KALFOU, NIGER.Msaada wa chakula waanza kuingia Niger
31 Julai 2005Matangazo
Msaada wa dharura wa chakula umeanza kuingia katika nchi ya Niger inayokumbwa na umaskini mkubwa pamoja na janga la njaa.
Ufaransa imelaumu maafa ya Niger yanayotokana na njaa kuwa yametokana na kuchelewa kwa jumuiya nzima ya kimataifa kuitikia kilio cha nchi hiyo.
Hapo jana waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Phillipe Douste-Blazy alisema Ufaransa sio nchi pekee yenye wajibu wa kuwasaidia Masikini Duniani.
Waziri huyo amesema nchi yake itaongeza maradufu msaada wa chakula kwa Niger hadi kufikia euro milioni 4.6 mwaka huu.
Idadi kubwa ya watoto wamefariki nchini humo huku baadhi ya wazazi wakiendelea kuishi bila chakula.
Wataalamu wanasema asilimia 30 ya idadi ya watu wa Niger wanakabiliwa na njaa