1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamala Harris aanzisha kampeni ya Urais 2024

22 Julai 2024

Makamu wa rais wa Marekani, Kamala Harris ameanzisha kampeni yake ya kutafuta kuungwa mkono, kuwania urais katika uchaguzi wa Novemba 5 mwaka huu. Wademokrat kadhaa tayari wamemuunga mkono mwanamama huyo.

Marekani | Kamala Harris | Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na Makomu wake Kamala Harris Picha: Andrew Harnik/Getty Images

Harris ameanza kutafuta uungaji mkono wa wajumbe wa chama chake cha Demokrats, muda mfupi, baada ya hapo jana rais Joe Biden kujiondowa katika kinyang'anyiro hicho kufuatia wasiwasi kuhusu umri wake na hali ya kiafya.

Rais Biden alitangaza pia kumuunga mkono makamu wake huyo kuwa mgombea urais wa Democrats. Taarifa zinasema kufikia sasa magavana kadhaa wenye sauti wametangaza kumuunga mkono kuwa mgombea urais atakayepambana dhidi ya mgombea wa Republican  Donald Trump.

Soma pia:Biden apongezwa kwa kujiondoa kwenye mbio za kuwania urais

Spika wa zamani wa bunge Nancy Pelosi na rais wa zamani Barack Obama wamempongeza rais Joe Biden kwa uamuzi aliochukua, wamejizuia hadi sasa kutangaza  kumuunga mkono Kamala Harris kuwa mgombea urais kwa niaba ya Democrats.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW